AT Asema WATANZANIA Wengi Na Wasanii Wakubwa Hawajui Msanii Bora Ni Yupi

0
193

Msanii wa miondoko ya mduara kutoka  visiwani Zanzibar AT amesema wabongo wengi na hata wasanii wakubwa wanajua msanii bora ni yule aliyefanya collabo nyingi na si kingine. AT ameiambia #planetbongo ya #EARADIO kuwa Watu hawana mahesabu ya kimuziki ya kuona msanii gani ana uwezo mkubwa kimuziki kuanzia show zake au utunzi ila wanaangalia yule maarufu na mwenye collabo nyingi.
Amesema hili ndilo linaongeza nyimbo Kali kutopewa nafasi na badala yke wale wenye uwezo Mdogo wanatoboa kirahisi.
AT aliwahi kunukuliwa akisema Mziki wa mduara haupewi nafasi kwasababu kuna ubaguzi kwakuwa Asili yake ni Zanzibar.

Facebook Comments